NA SALEH JUMA
Watanzania washauriwa kufuata uzazi wa mpango na uzazi salama
ili kupunguza ama kuondoa kabisa tatizo la watoto wa mitaani linalotokana na wazazi
kuto kumudu familia zao kwasababu ya hali
ngumu ya umasikini.
Hayo yamesemwa oktoba 25 na naibu waziri wa afya katika warsha
ya siku mbili ya wadau mbalimbali wa sekta ya afya iliofanyika katika baraza la
maaskofu kurasini jijini DAR ES SALAAM
“Wazazi na watanzania wenzangu tujitahidi kupanga uzazi salama
ili kupunguza kabisa tatizo la watoto wa mitaani kutokana na ugumu wa maisha tunashindwa kumudu familiazetu”
Aidha amewataka watanzania kujitokeza kupima virusi vya ukimwi
ili kujua afya zao na kuanza tiba mapema endapo amegundulika kuwa tayari
ameambukizwa virusi vinavyo sababisha ukimwi kwasababu serikali inatoa huduma hizo
bure bila malipo yeyote.
No comments:
Post a Comment