NA Daud Alex
Mwenyekiti wa mtaa wa Barabara ya mwinyi kata
ya Kiburugwa wilaya ya Temeke JUMA ALLY NGONYANI amepiga marufuku ya wakazi hao kutupa taka
katika eneo ambalo amekataza kutupiwa taka kwani huo ni uchafuzi wa mazingira.
Akiuzungumza na SAFARI 255 kwanjia ya simu
baada ya kamera ya safari 255 kuona taka hizo amesema kuwa tayari alikwisha
kuwaambia wananchi hao kuwa wasitupe taka eneo hilo lakini hata yeye
anashangazwa kuona wakizidi kutupa taka hizo.
Pia aliweka kamati ya ulinzi ili kuwazuia
watu wanao tupa taka katika eneo hilo lakini inaonyesha kuwa wameshindwa kazi
hiyo hivyo atavunja na kuunda upya kamati nyingine ili kuzuia hali hiyo kwani
niya hatari kwa afya zao.
Baadhi ya wakazi walio karibu na eneo hilo
wanasema kuwa hupatwa na harufu kali kutoka katika taka hizo hata wanapo jaribu
kulinda watu wasitupe taka katika eneo
hilo huwa hawawaoni majira ya mchana bali hukuta taka hizo wanapoamka
asubuhi.
Hata hivyo mwenyekiti wa mtaa huo amesema kuwa
yeye na wajumbe wake wataweka sheria kali ikiwamo kila atakaye kamatwa akitupa
taka katika eneo hilo atatoa faini ya shilingi elfu hamsini na kulisafisha eneo
hilo,vilevile ameongeza kuwa uchafu huo uliopo watahakikisha jumamosi ijayo
watafanya usafi kama agizo la mkuu wa mkoa wa Dar e s Salaam Poul Makonnda.
No comments:
Post a Comment