Thursday, 27 October 2016

MTOTO WA MIAKA 5 ABAKWA NA BABA YAKE MZAZI



Na Fadhila mohamed

     Jeshi la polisi wilayani kinondoni mkoani Dar es salaam linamshikilia mtu mmoja mkazi wa mwananyamala Khalid Mgeza mwenye umri wa miaka 25 kwa tuhuma za kumbaka mwanae wa kike Asha mgeza na kumsababishia maumivu makali. 



    Tukio hilo lilitokea tarehe 20 october mwaka huu katika kijiji cha mwananyamala wilayani humo ambapo baba huyo anafanyakazi katika eneo hilo na pia ni mkazi wa eneo lile.

     Kesi hiyo yenye namba NG2/LR/256 imefunguliwa katika kituo kidogo cha polisi na kupewa kipaumbele na  mwajuma na mama wa mtoto huyo khadija mwenda wanaifatilia kesi inayo mkabili mumewe kwa kufanya tendo hilo la ukatili kwa mtoto wake .


      Siku ya tukio kijana huyo anayefanya kazi ya ulinzi katika nyumba ya kulala wageni bondeni iliyopo mwananyamala alimchukua mtoto huyo na kwenda nae kazini kwake na ndipo tukio hilo kufanyika.

       Lakini baada ya kumrudisha nyumbani mama wa mtoto aliona mabadiliko kwa mwanae na kutoa tamko la kumpa adhabu kali kwa mtuhumiwa.ndipo kumchukua na kwenda nae hospital kw ajili ya vipimo zaidi ndipo daktari akithibitisha kubakwa kwa mtoto huyo”alisema Daud mjuni dokta wa kituo”


Hii ni picha ya mtoto aliyebakwa


    Kitendo hicho kinahusishwa na imani za kishirikina na matumizi ya madawa ya kulevya kutokana na uhalisia wa eneo la mwananyamala kuwa na tabia kama hizo ,huku serikali ikisisitiza kuacha  vitendo vya ukatili .






No comments:

Post a Comment