Thursday 27 October 2016

TSJ WATISHIKA KWA ELFU SABA

 Na
  Mary Peter

Wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari Time school of journalism (Tsj) kilichopo jijini Dar es salaam Ilalabungoni wameshangazwa na bei ya chakula walio ikuta Tanga korogwe wakiwa njiani Kwenye  safari yao ya masomo wakiwanjiani na maoni tofauti tofauti kuhusiana na bei ya vyakula katika ziara yao ya kuelekea  Arusha kufatia bei ya vyakula kuwa juu tofauti na mategeo yao
Baadhi ya wanfunzi wakiwa wanafuzi wakiwa wanapata chakula

Wakizungumza na mwandishi wetu kwa nyakati tofauti tofauti wanafunzi hao wameeleza kuwa walipelekwa kula sehemu ambayo bei ya chakula ipo juu ambapo sahani ya chakula in elfu 3,000 hadi elfu 7,000 na kupelekea wanafunzi kutumia pesa nyingi kwa ajili ya chakula nawengine kishindwa kuimudu bei hiyo wakiwa njiani korongwe Mkoani Tanga kuelekea  Mkoani Arusha.
hili ndio jengo la kilimanjaro hotel linavyoonekana
Naye Maria kilua mwanafunzi wa diploma ya pili  katika chuo cha Tsj alisema kuwa " yaani kwakeli hii bei ya chakula nikubwa sana has a ukiangalia wengine tunatoka katika familia  za heo hae Alf kwa mlo mmoja tu elf saba sasa na baadae itakuwaje maana being ambayo niya kawaida na nimeizoa ni 2500-3000 "alisema kilua.

Omary Zongo mwanafunzi wa Diploma ya nne  katika chuo cha Tsj alisema kuwa wameshanga sana kwa being ambayo wameikuta katika mgahawa ule  na kwa tofauti na being ambayo wameizoea kwao na kitu cha tofaut sana ukilinganisha na uwezo wao walio nao.

Kwa upande wake walimu wa chuo hicho cha Tsj Bwn George Baltazari alisema kuwa walilazimika kwenda kula katika hoteli  hiyo kutokana na kubadilika kwa ratiba na pia wanafunzi kwa muda huo walitakiwa kupata chakula na kuahidi kuwa watajitaidi kutafuta sehemu ambayo itakuwa na bei za kawaida za chakula kama ambavyo wengi wamezoea na kulingana uwezo wao.
Baadhi ya wanafunzi waTsj wakiwa wanachukua chakula  katika hotel ya kilimanjaro picha na Mary peter

Pia Makumu wa Rais wa chuo cha Time school of journalism (Tsj)Fatma sultan  naye alisema kuwa tumelazimika kuwaleta katika mgahawa huu kula kutokana na mwingiliano wa ratiba na vilevile hoteli  hii ni sehemu ambayo mabasi mengi yanapitia hapa na abiria kupata chakula hivyo hatukutegemea kukuta  bei za vyakula kuwa juu kiasi hiki ila naahidi kutatua changamoto hii.

No comments:

Post a Comment