Tamriha
Hamisi
Dar
es salaam
Wakazi wa mtaa wa
malapa buguruni jijini Dar es salaam wamelalamikia baadhi ya nyumba zilizopo
maeneo hayo kutiririsha maji machafu yanayotoka maliwatoni (msalani yakiwa na harufu kali na watoto
hucheza katika maeneo hayo bila ya kujua kuwa ni madhara kwao.
Waliyazungunza hayo na
Safari 255 ilipotua kwenye maeneo hayo na kusema kuwa wanapata wakati mgumu
sana kwa kuwa ni jambo llililodumu kwa muda mrefu bila ya kupata suluhisho la
suala hilo.
Safari 255 ilijaribu
kwenda serikali za mtaa wa malapa ili kupata taarifa juu ya suala hili lakini hawakufanikiwa kukuta msemaji
mkuu wa ofisi hiyo, na walipogeuka upande wa wamiliki halali wa nyumba hizo
hawakuwa tayari kuongea chochote.
Pia wananchi hao
waiomba serikali ya mtaa huo kuhakikisha inatilia mkazo na kulisimamia sula
nhilo kwa nguvu na bidii zote ili kusaidia kulinda usalama wa afya zao na
watoto wao wasio jua chochote.
Safari 255 limeahidi
kufuatilia suala hili kwa bidii na kuhakikisha linapatiwa ufumbuzi na
linakwisha kabisa katika mazingira yanayowazunguka wakazi wa eneo hilo, na
kufanya jitihada na kumpa mwenyekiti wa eneo hilo.
No comments:
Post a Comment