Na Janeth frank
Ukosefu wa
sehemu ya kuhifadhi magari yanaingia
kuleta bidhaa na kununua bidhaa ndogondogo katika soko lililoko buguruni
manispaa ya ilala jijini dar es salaam
,imekuwa ni kero kubwa kwa wafanyabiashara wadogo wanakuja kununua bidhaa na
wateja wa kawida.
Baadhi ya wateja wanaoingia sokoni walieleza
kuwa mara nyingi gari linapoingia au kutoka pande tofautitofauti za soko hilo
watu hulazimika kusubiri gari lipite
ndipo watu waingie au kuwapisha makuli wanaokuwa wanatoa bidhaa ndani na
kupeleka nje kitu mda mwingine unaweza ukasukumwa na kuanguka
.
Lakini pia mmoja wa madereva wanaoingia
kuleta bidhaa sokoni hapo alisema kuwa kitendo hiki kina tupa wakati mgumu sisi
madaereva na akaotolea mfano ,kuwa sokoni mabibo kuna sehemu malum kwa ajili ya
parking na kushusha mizigo sokoni hapo na akaiomba serikali iige mfano huo
itakuwa vizuri sana.
Kutokana na hali hiyo wafanyabiashara
hao walitoa ombi kwa serikali uongozi wa
soko hilo kufanya utaratibu wa kutatua kero hiyo ya ukosefu wa parking.
No comments:
Post a Comment