Thursday 27 October 2016

WAFANYAKAZI WA KIWANDA CHA KIOO WAJIANDAA KUGOMA



NA REHAN SERAPHEE
 
       Wafanyakazi wa kiwanda cha kioo limited kilichopo jijini Dares salaam wamesema hawatohudhuhuria kikao kilichoandaliwa na uongozi wa kiwanda kitakachofanyika mwezi ujao katika ukumbi wa mlimani city,kama hawatopewa shahiki zao.

Wakizungumza na mwandishi wa gazeti hili ,baadhi ya wafanyakazi ambao hawakutaka kutajwa majina  yao,mmoja wao amesema ‘’kila tarehe tano ya kila mwezi uongozi wa kiwanda hutupatia pesa za kujikimu lakini sasa ni miezi mitatu imepita bado hatujapewa pesa hizo za kujikimu’’. 
MMOJA WA WAFANYAKAZI WA KIWANDA KIOO LIMITED JINA LIMEIFADHIWA

Ameongeza kwa kusema kuwa hakuna dalili za uongozi wa kiwanda kuwasiliana na wafanyakazi ili kijua nini kimechosababisha tusipewe pesa zetu,vinginevyo sisi tutagomea kuhudhuria kikao hicho.
Naye mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi tawi la kioo limited ,Ally salumu amewataka wafanyakazi wa kiwanda hicho kuwa watulivu kwani wanalitambua tatizo hilo na linashughulikiwa ili kuweza kupata haki yao msingi kabla ya kikao kilichopangwa .
Baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda wakijadiliana namna ya kupaata atahiki zao

Nao uongozi wa kiwanda hicho kupitia meneja rasilimali watu ,William bongo alisema kuwa zoezi la kuhakiki majina ya wafanyakazi litachukua muda mrefu kwani uongozi umegundua kuna baadhi ya wafanyakazi siyo halali hivyo wafanyakazi wawe na imani na  utawala na haki zao watazipata ndani ya wiki moja ijayo kabla ya mkutano huo.
Pamekuwa na tetesi kuwa idadi ya wafanyakazi ni kubwa kuliko mahitaji ya kiwanda hivyo shughuli za uzalishaji hufanyika kwa zamu tatu yaani subuhi,mchana na usiku.

wafanyakazi wa kioo limited wakijiandikisha majina yao


No comments:

Post a Comment