Na imani luoga
Jengo la biashara maalumu kwa wafanyabiashara wadogo
wadogo maarufu kama Machinga Complex lililopo katika wilaya ya ilala Jijini Dar
es salaam tangu kukamilika kwake mwak 2013 limekuwa kivutio kikubwa kwa wafanyabiashara
na wateja mbalimbali wanaotembelea soko hilo
,
Tangu kukamilika kwake changamoto mbalimbali
zimejitokeza katika jengo hilo ikiwemo kuungua kwa jingo hilo, mgomo wa
wafanyabiahsra kuhamia katika jingo hilo, lakini zaidi Malalamiko kutoka kwa
wafanyabiahsra mbalimbali wenye matatizo ya ulemavu wa aina mblimbali.
Mwishoni mwa mwaka 2015 idadi kubwa ya walemavu
waliweka mgomo kuitaka serikali iwapunguzie kodi pamoja nakuwapatia vizimba vya
biashara maeneo ambayo yana muamko mkubwa wa biashara.
Mwaka mmoja sasa umepita tangu mgomo ule upite,
Chipukizi inaona haja yakufuatilia sakata hilo kwa kina nkuojua je limeisha
kama serikali ilivyo ahidi au bado kuna changamoto zinaendelea kujitokeza.
Salim Ahmud ni mwenyekiti wa chama cha
wafanyabiashara wenye ulemavu ambaye yeye ni mlemavu wa ngozi “Sio kwa kiwango
tulichohitaji” Anasema Salim, “ Serikali yetu ya mkoa inatekeleza ahadi kwa
mwndo wa kinyonga sana, ingawa tunashukuru baadhi yetu wamefanikiwa kupata
vizimba kariakoo lakini sisi wachche tuliobaki hapa tunakutana na changmoto
mbalimbali, kwa watu wenye mattizo ya viungo n hasa miguu, jingo hili sio
rafiki kabisa nawao”
Machinga complex imejengwa kwa mtindo kwa ghorofa,
kwa mujibu w Sali Anasema inawawia ngumu walemavu wa miguu na mikono kuweza
kupanda juu kwa ajili ya biashara “ Hii sio tu kwa wafanyabiashara wenye
ulemavu, bali hata kwa wateja wenye ulemavu ni ngumu kwa wao kupanda juu
kununua au kuuza bidhaa
”
Anaeleza Salim huku akionesha muundo wa soko hilo,
chipukizi linafanikiwa kuona vizimba vya biashara vilivyotengwa maalumu kwa
ajili ya watu wenye ulemavu lakini vingi vinaonekana kufungwa kwa mujibu wa
Salim anasema wamelazimika kufanya hivyo sababu ya ugumu wa biashara, mitaji
midogo na changamoto z upatikanaji wa malighafi “wengi wanaoendelea na kazi
hapa ni wale wenye ujuzi mbalimbali kama vile mafundi viatu na vifaa vya umeme,
kwa sababu mitaji yao ni ujuzi wao”
No comments:
Post a Comment