Na.Husna Kyelula
Baada
ta kutokuwa na muendelezo mzuri wa matokeo katika ligi kuu bara timu ya Azam
kupitia kwa mtendaji wao mkuu Sady Kawemba alisema kuwa sasa wameshtuka.
Kawemba
alisema kuwa wameshatuka na kwa nini wamekuwa na muendelezo mbaya wa matokeo katika
timu yao ambayo wameaanza nayo msimu huu chini ya kocha kutoka Hispania.
“Naweza
kusema kuwa tumeshtuka kwanini tunakuwa na matokeo ambayo siyo ya kulizisha kwa
mechi nyingi za ligi kuu bara ambalo tatizo hilo ni kwamba wachezaji wetu
wametumika sana wamechoka”alisema
“Kwani
ukiangalia wachezaji wetu wa kikosi cha kwanza wengi sana wametumika kwa muda
mrefu bila ya kuwa na mapumziko ya kutosha huku wengine wakishindwa kabisa
kuendelea na timu kwa kuwa wamepata majeraha ambayo yaliwawaka nje”alisema
“Kwa
sababu hiyo tumeshtuka kuwa uchovu wa wachezaji ndio unaotufanya kupata matokeo
haya mabayo kwa upande wetu siyo ya kulizisha lakini kwa kuwa tatizo tumeshalijua
tinakwenda kulifanyia kazi”alisema
Azam
watakuwa na kibarua kingine kigumu siku ya kesho katika uwanja wa Kaitaba
Bukoba kuwakabiri Kagera Sugar ambao nao wanaangaika kupata matokeo mazuri na
wakiwa na kumbukumbu ya kupingwa mabao sita dhidi Yanga.
Safi sanaaaaaaaa
ReplyDelete