Na Hamisa mkongo
Wakazi wa
buguruni katika wilaya ya ilala jijini Dar es salaam wameipongeza hatua ya
serikali ya kukamilisha kivuko cha daraja katika eneo la sheli kwani
kumewasaidia kupunguza ajali za mara kwa mara zilizokua zikitokea katika eneo
hilo
Akiongea na
chipukizi mapema hii leo mmoja wa wakazi na watumizi wa kivuko hicho Albert
Jumaalieleza furaha yake juu ya hatua ya serikali kusikiliza kilio chao cha
mda mrefu “Naishukuru sana serikali yetu chini ya mheshimiwa rais John Maufuli
kwa kuskiliza kilio chetu kwani tumekua tukitaabika sana wakati wa kuvuku huku
magari yanapita” alisema Juma aidha juma amewaombawakazi wenzake kulitumia
daraja hilo kama kivuko ili kuepusha ajali “Nawaombawakaziwenzangutulitumie
daraja kuvukia ili tuepukanae na ajali” alisistiza juma
Naye mmoja
wa madereva wanaotumia wanaotumia barabara hiyo Musa Hussein ameliambia
chipukiza kuwa wao kama madereva imewasaidia kuendesha gari kwa usala na
utulivu kutokana na uwepo wa daraja hilo linalotumiwa na watu na kusababisha
kupungua kwa foleni “kwa upande wetu imetusaidia kuendesha gari bila hofu na
pia foleni imepungu tunashkuru” alisema Hussein
Hatua ya
serikali ya kueka daraja katika eneo hilo imepongezwa sit u na wakazi bali
wadau kutoka sekta mbalimbali kwani kumepunguza ajali za mara kwa mara
zilizokua zikitokea katika eneo hilo.
No comments:
Post a Comment