LENYE MWANZO HALIKOSI KUWA NA MWISHO
by
Shinuna Nassir.
Hatimaye ule wakati uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu umefika, wanafunzi wa diploma ya nne ndani ya chuo cha uandishi wa habari Time school of journalism wanajiandaa kufanya mtihani wao wa mwisho ikiwa ndio kikomo cha daraja hilo walilofikia tayari kuvuka kwenda ngazi ya chuo kikuu.
Akizungumza na gazeti letu la chipukizi bw.Omar Zongo kutoka diploma ya nne alisema kuwa kilichobaki ni kumalizia hatua yao ya mwisho na kuachia wengine waweze kukamilisha safari yao pia kwani "lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho"
aliongezea kwa kusema mwisho upo kwa kila jambo ukianza japo katikati kuna kuwa na harakati za hapa na pale lakini mwisho wa yote ni kuvuna alichokipanda muhusika, alisema kusoma ni hatua muhimi katika maisha na ukifika tamati ya hatua basi ndo mwanzo wa hatua fuata.
aidha wazir wa elimu bw.Hans Mwaisemba alisema anatoa pongezi kwa wahitimu watarajiwa kwani ni hatua kubwa walio ifikia na kuwatakia kila la kheri katika mtihani wao wa mwisho vile vile aliwasihi kuendelea na masomo pale fursa zinapojitokeza bila kusahau kuwatenezea njia wadogo zao walioko vyuoni.
Pia bw.Prosper Kaijage ambae nae ni mtahiniwa mtarajiwa aliahidi mbele ya wanafunzi kadhaa kuwa mfano bora kuitumia taaluma yake vizuri ili kuwahamasisha wengine walioko TSJ na hata vyuo vingine vya jirani, vile vile aliwasisitiza kuwa wavumilivu, kujituma, na kutokata tamaa
Sanjari na maandalizi yao mratibu wa masomo bi Blandina Semaganga alisema"ni hatua ya mwisho kabisa kwa wahitimu kwani wataweza kujua uwezo wao na juhudi zao toka walipo ianza elimu hii ya kati kwani mafanikio hutegemea msingi uliokuwa imara hivyo basi kila mtu anajua anachokwenda kukifanya ni kipimo cha mwisho"lakini zaidi ya yote aliwatakia kila la kheri katika mtihani wao
Thursday, 27 October 2016
KILA LENYE MWANZP HALIKOSI KUWA NA MWISHO
Labels:
ZA NDANI YA CHUO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment