NA Daud alex
Vijana wa mtaa
wa kilungule kata ya kilungule jimbo jipya la mbagala wameiomba serikari ya
mtaa wao kuwaunga mkono katika mchezo wa mpira wa miguu ili waweze kukuza
vipaji vyao katika mchezo huo kwani unapendwa na vijana wengi.
Akizungumza
mmoja wa vijana wa mtaa huo Majidi nduli ameiambia safari255 kuwa katika mtaa
wa kilungule kuna viwanja vitatu ambavyo vyote hujaa wakati wa jioni kwa
kufanyiwa mazoezi ya mpira wa miguu hivyo hiyo ni ishara kuwa mchezo huo unapendwa
sana.
Aidha kwa
upande wao wakazi wa mtaa huo wamesema kuwa vijana wengi wanapenda mchezo huo
hivyo wanaiomba serikali ya mtaa wao kufanya jitihada za kuhakikisha wanawaunga
mkono vijana ili kuweza kuwaepusha na
vishawishi ambavyo vitawatia hatarini.
Kwa upande
wake mwenyekiti wa mtaa huo Barnabas Kayuni amesema kuwa serikali yake
imejipanga ipasavyo ili kuyaomba mashirika binafsi pamoja na wananchi wa mtaa
huo kuanzisha ligi mbalimbali ili waweze kufanya uhamasishaji kwa vijana hao
kwani serikali ya mtaa huo peke yake haitaweza.
No comments:
Post a Comment