Na Hamisa mkongo
Wakazi wavingunguti katika
wilaya ya ilala jijini Dar es salaam wamelalamikia mazingira machafu husussan
katika maeneo ya spenko wakidai kuwa hali hiyo inahatarisha maisha na
kusababisha maambukizi ya magonjwa kutokana na mtiririko wa maji machafu kotoka
katika viwanda hivyo.
Akionesha hisia zake mmoja
wa wakazi wa eneo hilo Asia Rashid wakati wa mahojiano maalum na gazeti la
chipukizi mkaazi huyo alieleza kuwa wana hofu ya kupatwa na magonjwa kutokana
na hali ya uchafu kukithiri “tunahofia kupata magonjwa kwa sababu ya maji
machafu yanayotiririka katika viwanda hivi apa vingunguti” alisema Asia.
Kwa upande wake mmoja wa
wafanyakazi wa viwanda hivyo Issa Ali aliliambia chipikizi kuwa mindombinu
mibovu katika viwanda hivyo ndio miongoni mwa sababu zinazopelekea uchafuzi wa
mazingira “viwanda vyetu vimekuwa na miundombinu mibaya ndio maana kunakosekana
sehemu yakupeleka maji taka” alisema Ali.
Licha ya juhudi za
chipukizi kuwasaka wakuu na wasimamizi wa viwanda hivyo lakini juhudi zao
hazijafua dafu.
Kero za maji taka kutoka
kwenye viwanda nchini nchini limekua tatizo sugu huku kidole cha lawama
kikielekezwa kwa serikali kwakulifumbia macho swala hilo.
No comments:
Post a Comment