Friday 28 October 2016

MKUBWA FELLA AJA NA YAH TMK MODERN TAARAB



NA SALEH JUMA
Kituo cha mkubwa na wanawe kilichopoTemeke jijini DAR ES SALAAM hivi karibuni kimeunda bendi mpya ya miondoko ya taarabu inayofahamika kama YAH TMK MODERN TAARABU iliyopo chini ya mkurugenzi Saidi Fella.
 
Fella amesema aliamua kuunda bendi ya taarabu baada ya kuona wasanii wazuri na wakali kutoka bendi ya jahazi modern taarabu kujiengua katika bendi hio hivyo aliona ili kuendeleza mziki wataarabu na kuendelea kuutangaza nje ya nchi ni vyema kuunda bendi ikiwa ni moja njia ya ajira kwa vijana hao pia kuutangaza mziki huo.

Aidha aliwataja wasanii walio jiengua katika kundi la jahazi na kuunda bendi mpya ya ya yah modern taarabu kuwa ni Fatma Mahmod (mcharuko), Aisha vuvuzela,Chidy boy, Kichupa, Mussa Mipango na Mohamed Mauji pia wasanii wengine waliojiunga na bendi hio kutoka bendi nyengine tofauti ni Maua Tego na Omary Tego ambao awali walikua wanaunda kundi la Coast Modern Taarab.
 
Pia amewaomba watanzania kuipokea kwa mikono miwili bend yake hio mpya na kutoa sapoti ya kutosha kwa kununua kazi zao kuomba katika media tofauti nyimbo zao kucheza na kujitokeza kwa wingi katika maonyesho yao.
 
Lakini pia amewa ahidi kuwapatia burudani za kutosha watanzania kwani bendi tayari ipo kambini na tayari wameshaingia studio kurekodi  nyimbo mbili ambazo mwisho mwa wiki hii zitaanza kusikika katika media tofauti.



No comments:

Post a Comment