Thursday 27 October 2016

KIJANA MHITIMU CHUO KIKUU AJIAJIRI



NA Rehan Seraphee

Kijana aliyehitimu chuo kikuu cha Dodoma mwaka 2014 Hamis salahe mkazi wa Buza jijini Dares salaam ameamua kujiajiri baada ya kuona vijana wengi wahitimu wa vyuo vikuu nchini wamwkosa ajira.
Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili hamis salehe ambaye pia amebobea masuala ya uchumi amesema’’anashangaa kuona vijana wengi wakilalamikia serikali na kusema hakuna ajirapindi wamalizapo vyuo mbalimbali hapa nchini’’ ameongeza kwa kusema vijana wasisubiri zjira kutoka serikalini badala yake wajitume kwa kufanya shughili mbalimbali.
Muuza duka la vifaa vya simu Jamis salehe akiwa ndani ya duka lake
Hamis salehe ambaye amefungua duka la vifaa vya vifaa vya simu amesema ‘’ilikuwa vigumu kwa mara yake ya kwanza kuanzisha biashara hiyo lakini ugumu wa maisha ndiyondiyo sababu yake kuu ya kuanzisha duka la vifaavya simu kwa sasa maisha ni mazuri tofauti na mwanzoni baada ya kutoka chuoni.ameshangaa pia kuona vijan wengi wakilalamikia kiwango cha mishahara kutoka katika taasisi mbalimbali za binafsi kuwa hazikidhi maitaji yao.
Vifaa vya simu ndani ya duka la Hamis salehe

Mteja aliyefika katika duka la selehe aliyejulikana kwa jina moja la Hadija amesema kuwa Hamis salehe ni kijana anayejitambua kwani anafanya shughuli zake kwa umakini na anawajali wateja wake .Hadija pia kaoneza anamtambua Hamis salehe kwa umakini na ubunifu wake wa kufanya shughuli mbalimbali za kimaendeleo

Haimi amewashauri vijana wanaitimu vyuo vikuu nchini Tanzania kujishughilisha na mambo ya kijami ikiwemo suala zima la ufanyaji biashara kwa ubunifu na kubuni miradi midogomidogo ili kuweza kujikwamua katika maisha haya magumu. 
Hamis salehe akiwa ndani ya duka la simu kwa matengenezo

No comments:

Post a Comment