Na
Samiri Mwegero
Ni muda mrefu tangu wakazi wa maeneo ya
Ilala ĵijini Dar es salaam ŵamekuwa wakilalamika juu ya swala la kukosa alama
za kivuko cha watembea kwa miguu maarufu (zebra) katika barabara ya uhuru
maeneo ya chuo cha uandishi wa habari (Tsj) hasa katika kituo cha msaada
garage.
Hivyo serikali imesikia kilio cha wakazi
hao na kuweza kufanikisha kuweka alama ya kivuko (Zebra) ili kuepusha
malalamiko pamoja na ajali za mara kwa mara zinazotokea katika eneo hilo.
Sameer Kassimu mwegero ni mmoja ya wakazi
waishio katika maeneo hayo alisikika akizumzungumza maneno haya alipohojiwa na
mwandishi wetu “ Tunashukuru sana kwa serikali kusikia kilio chetu na kuweza
kufanikisha suala kuweka alama za kivuko japokuwa kuna uhitaji wa kuweka tuta japo
moja ili kuimarisha usalama katika eneo hilo”.
No comments:
Post a Comment