Na Maria
Kilua
Shule ya
msingi Laibon iliyopo wilaya ya Munduri mkoani Arusha inakabiliwa na tatizo la
maji hali iliyopelekea wanafunzi hao kutopata huduma ya chakula kwa zaidi siku
tatu hali inayopelekea ufauru kuwa mdogo.
Wakati serikali
ya awamu ya tano ikionekana kutoa nguvu zake nyingi katika swala la elimu kwa
kuja na mchakato wa elimu bure ili kuhakikisha kila mtoto wa mtanzania analata
elimu.
Hali hii
imeonekana kushindwa kuzaa matunda kwa shule hii kwani pamoja na kupata elimu
bure shule hiyo imekuwa ikikoowa miundombinu ya maji na hatimaye watoto
kufikisha hadi nusu hadi wiki bila kupata chakula.
Akizungumza
na waandishi wa habari kutoka Chipukizi mwalimu mkuu wa shule hiyo ROGATH MBUYA
ameiomba serikali kuitazama kwa jicho la pili kwani tatizo hilo halipo kwa
wanafunzi tu bali hata walimu pia.
Licha ya
changamoto wanzokutana nazo watoto hao bado wana ndoto na lengo makubwa kama
vile udaktari, urahisi na mawaziri lakini ndoto hizo zimekuwa zikififia kila
uchwao kutokana na changamoto wanazokumbana nazo katika masomo yao.
No comments:
Post a Comment