Na Fadhila
mohamed
Jeshi la
polisi wilayani kinondoni mkoani Dar es salaam linamshikilia mtu mmoja mkazi wa
mwananyamala Khalid Mgeza mwenye umri wa miaka 25 kwa tuhuma za kumbaka mwanae
wa kike Asha mgeza na kumsababishia maumivu makali.
Tukio hilo
lilitokea tarehe 20 october mwaka huu katika kijiji cha mwananyamala wilayani
humo ambapo baba huyo anafanyakazi katika eneo hilo na pia ni mkazi wa eneo
lile.
Kesi hiyo
yenye namba NG2/LR/256 imefunguliwa katika kituo kidogo cha polisi na kupewa
kipaumbele na mwajuma na mama wa mtoto
huyo khadija mwenda wanaifatilia kesi inayo mkabili mumewe kwa kufanya tendo
hilo la ukatili kwa mtoto wake .
Siku ya
tukio kijana huyo anayefanya kazi ya ulinzi katika nyumba ya kulala wageni
bondeni iliyopo mwananyamala alimchukua mtoto huyo na kwenda nae kazini kwake
na ndipo tukio hilo kufanyika.
Lakini baada
ya kumrudisha nyumbani mama wa mtoto aliona mabadiliko kwa mwanae na ndipo
kumchukua na kwenda nae hospital kw ajili ya vipimo zaidi ndipo daktari
akithibitisha kubakwa kwa mtoto huyo”alisema Daud mjuni dokta wa kituo”
Kitendo
hicho kinahusishwa na imani za kishirikina na matumizi ya madawa ya kulevya
kutokana na uhalisia wa eneo la mwananyamala kuwa na tabia kama hizo ,huku serikali
ikisisitiza kuacha vitendo vya ukatili
na kutoa tamko la kumpa adhabu kali kwa mtuhumiwa.
No comments:
Post a Comment