Wednesday, 26 October 2016

ZOEZI LA UFUNGUZI WA BLOGG KWA DIPLOMA YA PILI LAKAMILIKA


Na Fadhili Kijanjali
TSJ
Zoezi la ufunguzi wa blogg kwa diploma ya pili  lilikuwa likiendelea chini ya usimamizi wa mwalimu wa online limemalizika rasmi hapo jana baada yakuchukua kipindi cha mda wa wiki mbili.
wanafunzi wa diploma ya pili wakisiliza maelekezo kutoka kwa mwalimu wa somo katika darasa la basata
 

Blogg hiyo ambayo imepewa jina la Safaritz255 imekamilika rasmi hapo jana nakuanza kufanya kazi rasmi huku wanafunzi wa diploma ya pili wakionesha kufurahia kumalizika kwa zoezi hilo ambalo lilikuwa na ugumu kwao.
Wanafunzi wa diploma ya pili wakiendelea na zoezi lakufungua blogg katika darasa la basata



Badhi ya wanafunzi wa diploma ya pili wamesema kufunguliwa kwa blog hiyo itakuwa ni chachu ya wao kufanya kazi kwa kasi ili waweke habari katika blog hiyo na watapata uzoefu utakaowasaidia hapo baadae.
Mtaalamu wa mambo ya IT ambaye pia ni mwana darasa Christian John akitoa maelekezo kwa wana darasa


Wamesema wanaamini kuwepo kwa blogg hiyo ni moja ya mazoezi ya vitendo watakayoyapata ndani ya chuo wakati wa kiendelea na masomo na kuongeza kuwa hata baadae watakapo maliza masomo yao tayali watakuwa na uwezo wakuendesha blog zao binafsi.
Wanafunzi wa diploma ya pili wakishangilia kwa pamoja baada yakukamilika kwa blogg iliyopewa jina la SAFARI 255


Blog ya Safaritz inategemea kufanya kazi wakati wote huku ikujumuisha habari za kitaifa, michezo na burudani, habari za biashara na habari za ndani tya chuo na haitakuwa na habari za kimataifa kwakuwa habari nyingi ni zitakazotoka katika maeneo ya karbu.

No comments:

Post a Comment