Thursday, 27 October 2016

SERIKALI YA WAJALI WANANCHI

  Na Yasinta Mkonyi  
Serikali ya Tanzania imekuwanikibuni mbinu mpya mbalimbali ili kuwasaidia wananchi wake. Swala la usafiri  jijini Dar es salam limekuwa kitovu kikubwa cha kero kwa wakazi wake

Miaka ya nyuma wakazi was jiji la Dar es salaam walikuwa wamezoea usafiri mmoja unaofahamika kama daladala wakwenda  pande zote za jiji la Dar es salaam. Usafiru huo ulikuwa ni was tabu kutokana na ongezeko la watu linalotokea Siku hadi siku. Na kufanya usafiri huo umekuwa wa shida  kwa baadhi ya maeneo kama vile Gongo la Mboto, Mbagala,Mbezi, Kimara na kadhalika
Kwa kuliona hilo serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania uliamua kuanzisha mradi mpya was magari yaendayo haraka maarufu kama mwendo kasi yanayofanya safari zake kati ya Kariakoo, Magomeni, Ubungo, na Kimara. Vilevile serikali haikuwasahau wakazi wa Gongo la Mboto kwa kuwaletea treini inayofahamika kama treini ya Mwakyembe ili kuweza kutatua matatizo ya wananchi  kwa baadhi ya maeneo.

No comments:

Post a Comment