NA HIDAYA YUSUPH
Dar es salaam
Wakazi wa
maeneo ya buguruni malapa jijini Dar es salaam wamefurahia ukarabati wa mto unaoendelea katika eneo la buguruni malapa
ambao umekuwa ukisababisha mafuriko na mmomonyoko wakati wa mvua nakuleta adha kubwa kwa wananchi wa maeneo ya jirani.
Mwonekano wa mto wa buguruni malapa kwa sasa wakati ujenzi ukiendelea |
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti wamesema mto huo kwa mda mrefu umekuwepo bila
kufanyiwa ukarabati na imekuwa ni hatari kwao kwakuwa mara nyingi mto huo umekuwa ukijaza maji na mara nyingi kusababisha mafuriko katika maeneo hayo
Wamesema
wakati wa mvua kuwekuwa na kero za mto huo na umekuwa ukimonyonyoka kwaa
kasi zaidi pembezoni hali iliyokuwa
ikitishia kubomoka kwa nyumba zilizojengwa katika maeneo jirani na mto huo kwa miaka ya baadae.
Ukuta mpya unaojengwa kwajili yakuzuia mmonyonyoko kaatika maeneo ya jirani na makazi ya watu walioko jirani na mto huo |
Kwa upande
wake mwekiti wa eneo hilo amesema ni hatua kubwa kwa serikali kuanza kutimiza
ahadi walizotoa kwa wananchi nakuongeza kuwa tatizo ilikuwa ni ukarabati wa mto huo
kutowekwa kwenye bajeti zilizopita.
Amesema
ukarabati ni kwaajili yakuepusha adha ambazo zingesababishwa na mto huo
kwa miaka ya baadae hasa wakati wa mvua ikiwemo magonjwa na mafuriko ambayo ni
hatari kwa maisha ya wananchi.
magari yakiendelea na matengenezo katika mto wa buguruni malapa |
Wakati
safartz255 inajaribu kumtafuta mkandarasi wa daraja jitahada ziligonga mwamba
kwakuwa mkandarasi hakuwa tayali kuzungumza kuhusu ujenzi huo kwa sasa.
Alama za tahadhari katika eneo la ujenzi zinazowekwa na watu wa usalama na afya makazini |
No comments:
Post a Comment