Na
Victoria Patrick
Kamanda wa polisi kanda ya maalumu ya jiji la Dar es salaam kamanda Simoni Siro akiongelea
hali ya usalama jijini.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake,
jana amethibitisha hali ya usalama ni nzuri na jeshi hilo limethibiti vitendo
vyote vya uhalifu vilivyoibuka hivi karibuni.
Pia alizungumzia suala zima la vijana wanaojiita
panya road, wanaosumbua jamii kuwa linashughulikiwa kikamilifu.
“hawa panya road lazima tuwatie nguvuni hawawezi
kusumbua jamii”alisema kamanda siro
pia amevitaja baadhi ya vitendo vya uhalifu
vilivyokuwa vikitawala jijini humu kuwa ni pamoja na wizi, ubakaji na utapeli.
Aidha kamanda siro amesema jeshi hilo limeimarisha
ulinzi katika maeneo ya yote ya jijivhususani nyakati za usiku ili kukabiliana
na matukio ya uvunjifu wa amani.
No comments:
Post a Comment