Thursday 27 October 2016

TEMEKE MARKET WAWALAZA KAUZU FC BAO 3-1





NA.HAMISA MKONGO.

Temeke Market ni timu chipukizi ambayo imepata jina kutokakana na mechi za Ndondo CUP ambayo ligi zake zilimalizika mwezi Agust 2016 na kupata ushindi wa kombe katika kuingia fainali na kuwa mshindi wa kwanza katika mechi hizo.

Vile vile temeke market ilicheza mechi ya kirafiki na Kauzu Fc katika uwanja wa karume jijini Dar es salaam na kuwapa mshangao mashabiki wao kwa kuwalaza mbele kwa bao 3-1  ushindi katika mechi ya kirafiki.

Hata hivyo kwa upande wa mashabiki wa kauzu Fc walizungumza kuhusiana na kipigo hicho ni kutokana na mazingira na kutokujipanga kwa wachezaji lakini wanaimani na timu yao kwa asilimia kubwa kuwa mchezo mwingine watafanuya vizuri.
Mchezaji wa timu ya kauzu fc alizungumza na mwandishi wetu kwa kusema ni kweli wamefungwa na wamepata kujua nini wanatakiwa kuongeza katika kufanya mazoezi lakini pia ni jambo ambalo halitojirudia tena.

Kocha wa timu ya kauzu fc alisema wanahitaji ushirikiano Zaidi katika kuendelez vijana ili kufika mbali katika kulisakata soka la Tanzania na kupata fursa ya kucheza na timu kubwa ili kupata uzoefu katika viwanja vya nyasi na hiyo yote ilikuwa ni mara yao ya kwanza

Kocha wa  timu ya Temeke Market Mgaya Ally alimalizia kwa kusema anawapa mazoezi makali wanafunzi wake na anamatumaini ya kufika nao mbali ila wanauhaba wa viwanja na kuiomba serikali kuweza kuwaboreshea viwanja na kupata uzoefu ili kuweza kucheza na timu kubwa kama Yanga, Simba na nyinginezo.

No comments:

Post a Comment