Na Janeth frank
Baadhi ya
wakazi waishio buguruni katika manispaa
ya ilala jijini dare es salaam walia na miundo mbinu ya kupitisha maji taka
kati mtaa wa buguruni kisiwani ambapo
makazi ya watu yapo karibu na mtaro huo.
huu ni mtaro ambao umepita katika mtaa huo unaoelekea sukita picha na janeth frank |
Wakazi hao wamesema kuwa katika mtaa
huo wa buguruni kisiwani kuna mtaro mkubwa unaoelekea maeneo ya sukita , kitu
ambacho kinasababisha uchafuzi wa hali ya hewa kuwa mbaya hasa nyakati za usiku
kwa waishio maeneo ya karibu
.
Chanzo cha habari cha safaritz
kilizungumza na baadhi ya wananchi hao ,ambapo mmoja wao aliyejitambulisha kwa
jina la Harid juma alieleza kuwa mara nyingi baadhi ya wakazi helekeza mitaro
ya choo kati mtaro ambao unaelekeza maji
hayo maeneo ya sukita
.
Kwa upande wake Bi fatma Adam ambaye ni
mfanyabiashara wa vitafunwa kama maandazi ,alisema endapo mtaro huo
hautafunikwa utaleta madhara kwa watoto ambao hupenda kucheza karibu na mtaro
huo mda ambao wazazi wao wanapiokuwa kazini
.
Aidha bwn geofrey lyanga naye kwa
upande wake alieleza jinsi ambavyo
anakerwa na harufu mbaya ya mtaro huo na kuiomba serikali kufanya utaratibu wa
kufunika mtaro huo ,kwani unaweza kuwa ni chanzo cha magonjwa ya mlipuko.
Chanzo cha habari cha safaritz kilifanya jitihada za kuutafuta
uongozi wa hususani mwenyekiti lakini ziligonjwa mwamba, lakini mjumbe wa mtaa
huo alikiri kuwa amepokea malalamiko hayo kutoka kwa wananchi hao na alifikisha
kwenye uongozi wa juu.
No comments:
Post a Comment