NA MSAFIRI
MOHAMEDY
Kampuni Asman Ltd iliyokuwa imeshika tenda
za ubebaji takataka katika eneo la
vingunguti kombo wametelekeza takataka zilizokusanywa katika eneo moja ambalo
hutumiwa kwa kukusanyia taka hizo na wao huja kuzibeba kwa sababu ya wananchi
kugoma kutoa hela za kugharamia huduma hiyo.
Yamezungumzwa hayo leo na mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo na kusema kuwa
imewabidi wasitishe kutoa huduma hiyo kwa sababu kuwa idadi kubwa ya wananchi
wengi hawakotoa kiasi cha shilingi 1500 ambayo hutozwa kwa ajili ya huduma hiyo
kwa kipindi cha mwezi.
Mwenyekiti wa mtaa huo amesama kuwa wapo katika mazungumzo na
viongozi wa kampuni hiyo ili waendelee
na kukusanya taka katika eneo hilo ikiwa ni pamoja na kuongea na wananchi ili
wawe wanatoa pesa ya kulipia gharama hyo kwa wakati sahihi ili kuondoa mvutano
baina ya wananchi na kampuni hiyo.
Pia wanachi wanaoishi na maeneo karibu na
maeneo ambayo takataka zimetelekezwa waliuomba uongozi wa eneo hilo kulishughulikia
tatizo hilo haraka iwezekanavyo ili kukinga afya zao kwa sababu ya harufu kali
inayotoka kwenye takataka hizo.
Mwenyekiti
wa eneo hilo aliongezea jambo kwa kuwataka kuwa wasikivu na waelevu wanakuwa
wanatakiwa kuchangia au kujitolea kitu katika jambo lenye manufaa kwao na jamii
kwa ujumla.
Mpaka mwandishi wa habari hii inaondoka eneo
la tukio hapakuwa na makubaliano ya viongozi
wa mtaa na wale kampuni iliyoshika kazi ya kuzoa takataka katika eneo hilo.
No comments:
Post a Comment