NA NAJAT ATHUMANI.
Wanafunzi wa
chuo cha uandishi wa habari Time school of journalism (Tsj) kilichopo ilala
bungoni wemefurahishwa na kitendo cha serikali kuweka kivuko cha alama ya
pundamilia kwa waenda kwa miguu katika
barabara kuu ya uhuru waitumiayo kuendea chuoni hapo.
Aidha mwandishi
wetu ameshuhudia uwepo wa alama hiyo ya pundamilia katika eneo hilo na kupata
maoni kwa baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho cha uandishi wa habari juu ya
kuwepo kwa kivuko hicho.
Mmoja wa
wanafunzi wa chuo hicho Agustino Luambano alifunguka kwa kusema jinsi ya alama
ya kivuko hicho kinavyowasaidia hasa katika baadhi ya masomo ambayo wanayasoma
BASATA ambapo inawalazimu kuvuka barabara.
‘‘kwakweli
hiki kivuko kimetusaidia sana kwani mwanzo tulikuwa tunapata taabu kuvuka
barabara kwa kuhofia magari na pikipiki ambazo huwa zinakwenda kwa kasi sana,
sasa tunavuka pasipo shida yoyote” alisema Agustino Luambano mwanafunzi wa
chuo.
Naye makamu
wa rais wa chuo hicho Fatma Sultani alielezea juhudi walizotumia ili kuwekwa
kwa alama hiyo ya kivuko “ tulikuwa tunatamani sana kuwepo kwa kivuko na mara
nyingi tulikuwa tunakaa kikao pamoja na
walimu ili watusaidie kufikisha malalamiko yetu sehemu husika kwani ajali nyingi za wanafunzi kugongwa na
magari pamoja na pikipiki zimekuwa zikitokea, nashukuru serikali imesikia kilio
chetu na sasa tunapita kwa amani”.
Ni wiki
kadhaa zimepita ambapo palitokea ajali iliyosababishwa na dereva wa pikipiki
maarufu kama bodaboda kumgonga mwanafunzi wa chuo hicho ajulikanaye kwa jina la
HUSNA……. Aliyekuwa akivuka barabara kabla ya kuwekwa kwa alama ya zebra na kuumizwa vibaya hivyo kuwahishwa katika hospitali ya wilaya
ya ilala Amana kwaajili ya matibabu. Hivyo kuwepo kwa alama hiyo inaaminika
kuwa itapunguza ajali za mara kwa mara.
Kivuko cha alama ya zebra
kilichowekwa kwaajili ya kuwasaidia
wanafunzi na wakazi wa eneo la ilala msaada gereji kupita kwa usalama.
Wanafunzi wa chuo cha uandishi wa
habari (Tsj) wakiwa wanavuka barabara
katika kivuko kuelekea chuoni.
Wanafunzi wakipita barabarani bila
wasiawasi baada ya kuwekwa kwa alama ya kivuko katika eneo hilo.
PICHA NA NAJAT ATHUMANI.
No comments:
Post a Comment