Wednesday 26 October 2016

ABIRIA WALIA NA USAFIRI WA TRENI YA TAZARA


Na HIDAYA YUSUPH
Dar es salaam
Abiria wanaotumia usafiri wa treni ya tazara maarufu kama treni la mwakembe jijini Dar es salaam inayopiga masafa ya tazara mpaka Mwakanga wamelalamika nakusema treni hiyo sasa imekuwa kama daladala kutokana na ongzeko la abiria wanaotumia usafiri huo.
Baadhi ya abiria wakiwa kituoni tazara kwaajili yakusubili treni



Mmoja kati ya abilia hao anayefahamika kwa jina la Hassan Ally amesema kwa sasa ni wazi kuwa abiria wanaotumia usafiri huo wamekuwa wengi kuliko kiasi ambacho treni hiyo inaweza kumudu kutokana na hali ya usafiri kuwa ngumu.
Abiria wakielekea kupanda treni katika kituo cha tazara


Ameongeza kuwa mida ya asbuhi na jioni ndio wakati ambao hali inakuwa ngumu kwa watumiaji wa treni hiyo kwakuwa ndio mida ambayo watu huwa wanaenda nakutoka maeneo yao yakufanyia kazi hali inayofanya abiria kuwaa wengi
Abilia waliowahi kupanda kwenye tren wakiwa wameketi kwenye siti zao


Kwa upande wa baadhi ya watumishi wa treni hiyo ambao hutumika kwaajili yakukata tiketi za abiria wamesema kuwa kwa sasa hali ya kuongeza kwa abiria haikwepeki a inawapa wakati mgumu sana wakati wa utendaji wa kazi zao.
Abiria wakiwa wameshikilia bombo ndani ya treni


Jitihada za safari 255 kumtafuta mkuu wakituo cha tazara ili azungumzie sala hilo ziligonga mwamba kwakuwa hakuwa tayali kulizungumzia swala hilo nakudai kuwa tayali wakubwa wake wameshatoa matamko.

“Tunategemea kuboresha usafiri wa treni”. Ni maneno ya waziri wa uchukuzi na mawasiliano Makume Mbawala aliyoyatoa baada yakupata kilio cha wananchi kuhusiana na usafiri wa treni kulemewa na abiria.

No comments:

Post a Comment