NA SALEH JUMA
Kituo cha mkubwa na wanawe kilichopoTemeke jijini DAR ES
SALAAM hivi karibuni kimeunda bendi mpya ya miondoko ya taarabu inayofahamika kama
YAH TMK MODERN TAARABU iliyopo chini ya mkurugenzi Saidi Fella.
Fella amesema aliamua kuunda bendi ya taarabu baada ya kuona
wasanii wazuri na wakali kutoka bendi ya jahazi modern taarabu kujiengua katika
bendi hio hivyo aliona ili kuendeleza mziki wataarabu na kuendelea kuutangaza nje
ya nchi ni vyema kuunda bendi ikiwa ni moja njia ya ajira kwa vijana hao pia
kuutangaza mziki huo.
Aidha aliwataja wasanii walio jiengua katika kundi la jahazi
na kuunda bendi mpya ya ya yah modern taarabu kuwa ni Fatma Mahmod (mcharuko),
Aisha vuvuzela,Chidy boy, Kichupa, Mussa Mipango na Mohamed Mauji pia wasanii wengine
waliojiunga na bendi hio kutoka bendi nyengine tofauti ni Maua Tego na Omary Tego
ambao awali walikua wanaunda kundi la Coast Modern Taarab.
Pia amewaomba watanzania kuipokea kwa mikono miwili bend
yake hio mpya na kutoa sapoti ya kutosha kwa kununua kazi zao kuomba katika
media tofauti nyimbo zao kucheza na kujitokeza kwa wingi katika maonyesho yao.
Lakini pia amewa ahidi kuwapatia burudani za kutosha watanzania
kwani bendi tayari ipo kambini na tayari wameshaingia studio kurekodi nyimbo mbili ambazo mwisho mwa wiki hii zitaanza
kusikika katika media tofauti.